Ecclesiastes 10


1 aKama vile nzi waliokufa huacha harufu mbaya kwenye manukato,
ndivyo upumbavu kidogo huzidi nguvu hekima na heshima.

2 Moyo wa mwenye hekima huelekea kuume,
lakini moyo wa mpumbavu huelekea kushoto.

3 Hata anapotembea barabarani,
mpumbavu hukosa ufahamu
na kudhihirisha kwa kila mmoja
jinsi alivyo mpumbavu.

4 bKama hasira ya mtawala ikiwaka dhidi yako,
usiache mahali pako,
utulivu huweza kuzuia makosa mengi.


5 Kuna ubaya niliouona chini ya jua,
aina ya kosa litokalo kwa mtawala:

6 cWapumbavu kuwekwa kwenye nafasi nyingi za juu,
wakati matajiri hushika nafasi za chini.

7 dMimi nimeona watumwa wamepanda farasi,
wakati wakuu wakitembea
kwa miguu kama watumwa.


8 eYeye achimbaye shimo
aweza kutumbukia ndani yake,
yeyote abomoaye ukuta
anaweza kuumwa na nyoka.

9 fYeyote apasuaye mawe
inawezekana yakamuumiza,
yeyote apasuaye magogo
inawezekana yakamuumiza.


10 Kama shoka ni butu
na halikunolewa,
nguvu nyingi zinahitajika,
lakini ustadi utaleta mafanikio.


11 gKama nyoka akiuma kabla ya kufanyiwa uaguzi,
mwaguzi hatahitajika tena.


12 hManeno yatokayo kinywani mwa mtu mwenye hekima
yana neema,
bali mpumbavu huangamizwa
na midomo yake mwenyewe.

13 Mwanzoni maneno yake ni upumbavu,
mwishoni ni wazimu mbaya,

14 inaye mpumbavu huzidisha maneno.

Hakuna yeyote ajuaye linalokuja,
ni nani awezaye kueleza ni jambo gani
litakalotokea baada yake?


15 Kazi ya mpumbavu humchosha mwenyewe,
hajui njia iendayo mjini.


16 jOle wako, ee nchi ambayo mfalme wako alikuwa mtumwa
na ambayo wakuu wako hufanya karamu asubuhi.

17 kHeri wewe, ee nchi ambayo mfalme wako ni wa uzao wenye kuheshimika
na ambayo wakuu wako hula chakula kwa wakati unaofaa:
ili kupata nguvu na si kwa ajili ya ulevi.


18 lKama mtu ni mvivu paa la nyumba huinama,
kutokana na mikono milegevu, nyumba huvuja.


19 mKaramu hufanywa kwa ajili ya kicheko,
nao mvinyo hufurahisha maisha,
lakini fedha ni jawabu la mambo yote.


20 nUsimshutumu mfalme hata ikiwa ni katika mawazo yako,
au kumlaani tajiri katika chumba chako cha kulala,
kwa sababu ndege wa angani wanaweza kuchukua maneno yako,
naye ndege anayeruka anaweza kutoa taarifa ya yale uliyosema.
Copyright information for SwhKC